SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU NAMMA YA KUPATA CHAKULA CHA MSAADA

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amesema masuala ya upungufu wa chakula yanachukuliwa kama maafa kwa mujibu ya sheria ya maafa iliyopo nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akitoa ufafanuzi bungeni juu ya utaratibu wa kufuata ili kupata chakula cha msaada.(Picha na OWM).

Waziri ametoa kauli hiyo wakati akifafanua hoja iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, Mhe. Yahaya Ally Mhata Bungeni Februari 3, 2023 katika Mkutano wa Kumi Kikao cha Nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu taratibu za kufuata ili kupata chakula cha bei nafuu.

Alisema kuwa, ofisi yake ina jukumu ya kuratibu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa kushirikiana na sekta tofauti tofauti ikiwemo hatua zote muhimu za uzalishaji, upatikanaji hadi matumizi kwa walaji.

Alifafanua Ofisi ya Waziri Mkuu inajukumu la kutoa kibali kwa ajili ya chakula cha bei nafuu au msaada linaratibiwa kwa kuielekeza Wizara ya Kilimo kuchukua hatua kupitia NFRA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akiteta jambo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula.

“Kimsingi jukumu la kutoa chakula cha bei nafuu au msaada ni jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo inalitekeleza kwa kuelekeza Wizara ya Kilimo ili ielekeze NFRA kupeleka eneo la kukipeleka kile chakula na kwenda kukiuza kwa bei nafuu iliyopangwa,”alisisitiza Waziri Simbachawene.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news