Tanzania yajizatiti kutumia fursa zinazopatikana ndani na nje ya nchi kukuza uchumi

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kushirikiana na nchi mbalimbali duniani ili kukuza uchumi wa nchi kupitia fursa za biashara, uwekezaji na utalii zilizopo ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Bungeni leo Februari 9,2023 wakati akijibu swali la Mhe. Felista Njau, Mbunge wa Viti Maalum kuhusu umuhimu wa Serikali wa kuainisha nchi zenye fursa za biashara na uwekezaji ili kukuza pato la Taifa.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akijibu swali bungeni jijini Dodoma leo Februari 9, 2023.

Amesema, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Wizara za kisekta na Balozi za Tanzania imeendelea kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zenye manufaa kwa Taifa na kwamba Wizara inaandaa Mpango wa Kitaifa wa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi utakaojumuisha Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kufikia malengo tarajiwa.

Amesema, mpango huu ambao unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Desemba 2023, pamoja na mambo mengine unalenga kuhakikisha fursa za biashara, uwekezaji na utalii zinakuwa na tija zaidi kwa wananchi wa Tanzania. 

Pia Mpango huo utajumuisha Sekta zote husika ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo muhimu ya kisekta yatakayo changia katika kukuza uchumi na pato la Taifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akichangia hoja kuhusu Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi wakati wa kipindi cha maswali na majibu kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma leo Februari 9, 2023. 

Akichangia hoja kuhusu mkakati wa utoaji elimu kwa wananchi kuhusu dhana ya Diplomasia ya Uchumi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema Wizara inaendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali na kufafanua kwamba Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi unaoandaliwa pia utajumuisha Mpango wa kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana hiyo ili kuwawezesha wananchi kuielewa dhana hii na kuwawezesha kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.

Kuhusu taarifa hasi zinazotolewa na vyombo vya kimataifa dhidi ya Tanzania, Mhe. Dkt. Tax amesema tayari Wizara imeanza kushirikiana na vyombo vya habari vya Nje hususan vile vinavyorusha matangazo yake kwa Kiswahili ili kupitia vyombo hivyo fursa na taarifa chanya kuhusu Tanzania zitangazwe duniani kote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. mm pendekezo langu juu ya huu mkakati wa kuwasaidia vijana kwa kuwapa eka kumi kumi ili wakalime,ni jambo zr sana.na kama litasimamiwa vzr.ni ukweli baada miaka kadhaa uchumi wa nchi yetu utakuwa na kukuwa.isipokuwa kuna siku nilikutana na ile fomu ambayo kijana wa tanzania anatakiwa kuijaza ili aweze kupatiwa hizo eka kumi..kwa kweli fomu ile ni dalili kuwa kuna mchezo wa kurudisha nyuma hizi juhudi za mh rais ili zisifanikiwe.
    na hizi ni taarifa rasmi tunazitowa ili wale wenye uwezo wa kuzifikisha kwake wamfikishie.
    kama mh rais atakuwa na mda tunamuomba na yy aipitie ile fomu ya maombi kisha aitathimini yy mwenyewe ili aone kama kuna kijana wa kitanzania atakae qualify kupata hizo eka kumi.na pia aone kama kuna sida ya kuwa huyu kijana atakopesheka kutoka kwenye mabenki yetu.maanake kwa mm naona kwa masuali yale yaliopo kwenye ile fomu,naona kama serikali haipo seriuos juu ya jambo hili.maanake %kubwa sana ya vijana hawana elimu ya kilimo.na ni vijana waliofeli darasa la 7 miaka ya nyuma huko.sasa kijana huyu.mmm nahisi hata kuijaza tu hiyo fomu ki usahihi,hawezi….!

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news