WASHINDI WA MTOKO WA KIBINGWA NA BETIKA KUPATA TIKETI ZA NDEGE

NA MWANDISHI WETU

WASHINDI wa Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa ya Betika watapata fursa ya kuja jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Ndege (kwenda na kurudi) ili kushuhudia mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga utakaopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Aprili 16, 2023.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Februari 27, 2023, Afisa Habari wa Kampuni hiyo, Juvenalius Rugambwa amesema licha ya Washindi hao kupata tiketi za Ndege, pia watashuhudia mchezo huo wa watani wa jadi wakiwa wamekaa kwenye siti za VIP A katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa sanjari na kusindikizwa na king’ora pindi wanapokuja uwanjani.

Rugambwa amesema: “Washindi wa Promosheni hii ya Mtoko wa Kibingwa ya Betika, wale wa mikoani watapata fursa kuja Dar es Salaam kwa usafiri wa Ndege (kwenda na kurudi) kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo wa kihistoria, pia watakaa siti za VIP A na watasindikizwa na king’ora wakati wanakuja uwanjani na watalala kwenye hoteli ya yenye hadhi ya nyota tano.”

Amesema mpaka sasa Mabingwa kutoka mikoani waliojishindia ticket za ndege kuja kwenye Mtoko wa Kibingwa ni Bahame Masangwa Balele (Simiyu), Constantine Constantine Mbele (Ruvuma), Stephano Skaut Charles (Kagera), Joshua Charles Gasado (Mkuranga), (Salivius Lucas Frugence (Njombe).

Wengine ni Paschal David John (Geita), Jovin Joseph Rwakatale (Ilemela/Mwanza), Richard Moris Mbewe (Nkasi/Rukwa), Elias Ezekiel Msongole (Mbeya), John Nodi Nyato, (Njombe), William Athuman (Dar es Salaam), Joram Pius (Kagera), Said Mohammed (Moshi), Pius Mwanakatwe (Sumbawanga), Gwinar Fotinati (Njombe), Kennedy Ernest - (Ruvuma), Sharifu Mohamed (Mtwara).

Washindi wanapatikana kupitia droo za kila wiki huku kila wiki Betika ikitangaza zaidi ya Washindi 10, tarehe ya droo za wiki ni 27, 1, na 3, Machi 2023. Jinsi ya kushiriki kwenye droo, mshiriki anatakiwa kubashiri mikeka mitano, kila siku na hakikisha kila mkeka ana bashiri kwa dau la kuanzia Shilingi 500/- na kuendelea. Pia, mshiriki anaweza kubashiri kupitia Tovuti ya www.betika.co.tz au kwa kupiga *149*16#.

Hata hivyo, mkeka wako ukichanika au usichanike moja kwa moja mshiriki huyo anaingia kwenye droo ya Mtoko wa Kibingwa ambayo itakupa fursa kuja jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Ndege kushuhudia mtanange wa Simba v Yanga Aprili 16, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news