Waziri Dkt.Tax apokea hati za utambulisho za mabalozi wateule kutoka Zambia, Brazil na Vatican

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amepokea nakala za Hati za Utambulisho za mabalozi wateule wa nchi za Zambia, Brazil na Vatican.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Waziri Tax amepokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere, Balozi mteule wa Brazil nchini, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na Balozi Mteule wa Vatican Nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti Waziri Tax amewahakikishia ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ya kibalozi hapa nchini. Pia Waziri Tax ametoa rai kwa mabalozi hao kuendeleza na kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na nchi zao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tanzania na Zambia tumekuwa marafiki na ndugu wa muda mrefu, Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Zambia katika sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,” alisema Dkt. Tax

Balozi mteule wa Zambia nchini, Mhe. Mathew Jere ameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Zambia na Tanzania katika sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, pamoja na nishati.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Brazil nchini, Mhe. Gustavo Martins Nogueira katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Balozi Mteule wa Brazil, Mhe. Gustavo Martins Nogueira ameahidi kuwa Brazil itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mapya ya kimkakati kwa manufaa ya mataifa yote mawili hususan kilimo, biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Naye Balozi wa Vatican nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino ameahidi kuendeleza kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya Vatican na Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news