Yanga SC yasogelea ubingwa Ligi Kuu ya NBC

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga kutoka jijini Dar es Salaam ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wamesogelea ubingwa wa ligi hiyo yenye mvuto nchini.
Ni baada ya kuzoa alama tatu kupitia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.

Clement Mzinze ndiye aliyeweka nvayuni bao hilo dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo lililodumu hadi mapumziko.

Aidha,kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo katika dakika ya 75 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Clement Mzinze na kumwingiza Fiston Mayele huku Mudathir Yahaya akiingia kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya.

Kwa matokeo hayo Yanga inafikisha alama 62 ikitofautiana na Simba SC kwa jumla ya alama nane.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news