Asali ya Tanzania kuuzwa China

NA DIRAMAKINI

UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China umesema mkataba wa kuruhusu asali kutoka Tanzania kuingia katika soko la China utasainiwa hivi karibuni.

"Katika utekelezaji wa makubaliano ya kukuza biashara kati ya Tanzania na China yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Suluhu nchini China, mkataba wa kuruhusu asali kutoka Tanzania kuingia katika soko la China utasainiwa hivi karibuni na kufungua fursa kwa wafanyabiashara wa asali kuuza bidhaa hiyo nchini China,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Asali na nta ni moja ya mazao makuu ya nyuki nchini Tanzania, pia huzalisha nta. Tanzania ina mazingira mazuri ya kuzalisha asali kwa kiwango cha juu cha ubora kutokana na kuwepo kwa aina nyingi ya spishi za mimea inayozalisha chakula cha nyuki (mbochi na chavua).

Pia kutokana na sababu hizo, asali inaweza kupata soko lenye bei ya juu endapo tutadumisha ubora wake.

Asali hutumika kama chakula, dawa na zao la biashara. Aidha, asali hutumika kama kiambato muhimu katika uokaji, viwanda vya vyakula vitamu, vipodozi, vinywaji na viwanda vya dawa.

Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Machi 1998 na Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Novemba 2001, Tanzania huzalisha takribani tani 4,860 za asali.

Taarifa ya mwaka 2006 ya Idara ya Misitu na Nyuki inaonesha kuwa Tanzania husafirisha nje ya nchi wastani wa tani 500 za asali. Wanunuzi wakuu wa asali ya Tanzania ni nchi za Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Ubeligiji na Mashariki ya Mbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news