Dkt.Tumaini Msowoya aikumbusha jamii kuhusu malezi ya watoto

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Msowoya Foundation, Dkt.Tumaini Msowoya ameikumbusha jamii kuhusu malezi ya watoto.
Amesema, mmomonyoko mkubwa wa maadili unatokana na malezi hafifu ya baadhi ya wazazi na walezi kutokana na ubize wa kazi bila kukumbuka watoto wao.

Akizungumza na wananchi wa baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Dkt.Msowoya amesema, watoto wanaweza kuwa salama ikiwa watalindwa na kufundishwa maadili mema.

"Kuna haja gani kwako kuwa bize wakati mtoto wako anaharibika? Anafanyiwa ukatili wala huna habari? Ukirudi nyumbani hoi hata muda wa kuongea nae huna, tubadilike ndugu zangu. Tukienda shambani basi tukumbuke tuna watoto.
"Sisi Msowoya Foundation tutaendelea kutoa elimu kwa jamij yetu, malezi ya watoto ndio ambayo yanaijenga kesho yenye watu wastaarabu na wenye utu," amesema.

Dkt.Msowoya ni mwanaharakati wa haki za watoto, mwimbaji wa muziki wa injili, mwanahabari nguli na mwanasiasa akishika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news