TAMWA Zanzibar yabisha hodi shuleni

NA DIRAMAKINI

ZAIDI ya wanafunzi 300 kutoka shule mbili za wilaya ya mjini Unguja wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na kutambua viashiria vya udhalilishaji katika maisha yao ya kila siku.
Shule hilzo ni Memon ya Stown Town na Bubu ambapo maafisa wa TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na mitandao ya kupinga udhalilishaji (GBV network) wamekuna na kutoa elimu kwa wanafunzi hao kwa nyakati tofauti.

Wakati wakitoa elimu maafisa hao wakiongozwa na afisa anashughulikia maswala ya udhalilishaji TAMWA-ZNZ Zaina Salum amesema wameamua kuwafikia wanafunzi mashuleni kutokana na sababu mbali mbali.

Alisema kwa kipindi kirefu wamekua wakitoa elimu kupitia vyombo vya habari jambo ambalo wanadhani kuna wakati elimu hiyo haifiki kwa walio wengi na ndio maana kila leo matendo hayo yamekua yakifanyika.
"Unajua ukija huku field ndio haswa unakutana na watoto wenyewe ambao ndio wanaokumbwa na kadhia hii,na hatuna hakika kutokana na umri wao kuwa wanaskiliza redio au kusoma magazeti," aliongezea.

Pia aliwataka watoto hao kufanya vitu muhimu ambavyo wanapaswa kuvifanya sasa kutoka na umri wao ikiwemo kujikita zaidi katika elimu.

Mwawakilishi kutoka mtandao wa kupinga udhalilishaji Huda Gharib aliwataka wanafunzi hao kuwa makini sambamba na kuepuka makundi ya watu wasiowaamini hata mitaani mwao.
Pia aliwataka wanafunzi hao kutoacha kabisa kuwa na aina ya marafiki wasiokua wa umri wao kwani wanajua mambo mengi zaidi hivyo wanaweza kuwashawishi.

Kwa nyakati tofauti watoto hao walioneshwa kuguswa na elimu hiyo na kueleza kuwa wanapaswa kuifanyia kazi.

Mmoja wao Saida Awadhi aliwataka watoto wenzake kutoa taarifa kwa wazazi wao pale wanapoona mazingira hatarishi kwao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Matendo ya udhalilishaji yanapaswa kupigwa vita na watu wote, hongera TAMWA kwa juhudi munazozichukua

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news