Fedha za Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini zaelekezwa kwenye ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi

NA FRESHA KINASA

MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara umepokea shilingi milioni 75.8 na fedha zote hizo zimeelekezwa kwenye ujenzi na ukamilishaji wa Maabara za Masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia na Bailojia) kwenye Sekondari za Kata za Musoma Vijijini.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 17, 2023 na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini chini ya Mbunge wa jimbo, Prof.Sospeter Muhongo.

"Lengo letu la sasa ni Musoma Vijijini kuwa na High Schools 4-6 za Masomo ya Sayansi ndani ya miaka mitatu ijayo.Jimbo letu lenye kata 21, lina jumla ya sekondari 27. Kati ya hizo, 25 ni za kata kwa maana ya Serikali na mbili ni za madhehebu ya dini (Katoliki na Sabato).

"Leo, Ijumaa, tarehe 17.3.2023, Mwenyekiti wa Mfuko wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo (Mb) ameongoza Kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichogawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia fedha za mfuko huo.

Fedha za Mfuko huo zimetunzwa na halmashauri yetu (Musoma DC) na ndiyo itakayofanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi.Wakuu wa Shule za Sekondari zetu zote za Kata (25) wamekaribishwa kwenye Kikao hicho,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.


VIFAA VYA UJENZI VITAKAVYONUNULIWA

Jumla ya Fedha:

Tsh 75,796,000

Saruji Mifuko (50%)

1,613

Mabati (40%)

947

Nondo (10%)

337

VIGEZO VYA MGAO

Sekondari mpya zimepewa kipaumbele

Sekondari zisizo kwenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha zimepewa kipaumbele

Sekondari zilizoshindwa kutumia vifaa vilivyogawiwa huko nyuma havikugawiwa cho chote.

Sekondari ambazo wizi umefanyika hazikugawiwa cho chote.

MGAO WA VIFAA VYA UJENZI

(1) SARUJI MIFUKO

Muhoji (300)

Bwai (300)

Mkirira (200)

Mabui (200)

Mtiro (200)

Bukima (150)

Bulinga (150)

Ifulifu (100)

(2) MABATI Gauge 28

Seka (142)

Kigera (112)

Muhoji (110)

Bwai (110)

Busambara (104)

Bukwaya (100)

Mabui (92)

Suguti (62)

Bukima (62)

Makojo (50)

(3) NONDO mm12

Muhoji (50)

Bwai (50)

Seka (50)

Busambara (50)

Mtiro (49)

Kigera (48)

Bukwaya (40)

Kikao cha ugawaji wa vifaa hivyo hapo juu kimefanyika kwenye Ofisi za Muda za Halmashauri zilizoko Kijijini Nyang'oma, Kata ya Mugango

UPOKEAJI NA USAFIRISHAJI WA VIFAA VYA UJENZI

Siku ya Alhamisi ya Machi 23,2023,wakuu wa Shule za Sekondari na Bodi zao watasafirisha vifaa vya ujenzi walivyogawiwa kutoka Bohari ya Halmashauri yetu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news