Haya hapa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa wananchi

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amewaomba wakazi wa Jiji la Dodoma kuzingatia usafi wa mazingira kila siku ili kuliweka Jiji katika Hali ya usafi ili kuendelea kuipa hadhi na mvuto wa makao Makuu na kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Senyamule ameyasema hayo alipokagua usafi wa mazingira katika Kata ya Chamwino Jijini humo uliofanywa na wananchi wa kata hiyo katika mazingira ya ofisi ya kata hiyo.
"Nitoe wito kwa wanachamwino tuendelee kufanya usafi siku zote tusiwe tunangoja siku ya Jumamosi ili mji wetu uingie katika miji Bora sio tu Tanzania bali Duniani. Ninyi wananchi ndio mtakaofanya mji uwe nadhifu ili kufanikiwa katika hili inatakiwa tusitupe taka hovyo na kuzingatia kanuni zote za usafi na hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kutoa kwa wakati taka zinazokusanywa katika miji na kupelekwa dampo.
"Mji wa Dodoma Umepewa baraka ya kuwa makao Makuu ni lazima kila kitu kiwe kwa mpangilio na kuzingatia viwango vinavyokubalika katika majiji pia tuendelee kupanda miti ili kukijanisha Dodoma," amesema Senyamule

Aidha, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw. Dickson Kimaro amesema hadi sasa wamekusanya zaidi ya shillingi milioni moja kwa wale wote wasioshiriki katika zoezi Hilo.
"Kwa wananchi ambao hawatekelezi Sheria ya kufanya usafi huwa tunawatoza faini na hadi kufikia hii leo zaidi ya Milioni Moja zimekusanywa Kama faini kwa wale wote wanakutwa wakiendelea na shughuli binafsi muda ambao umetengwa kwa ajili ya usafi,"amesema Kimaro

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwaja ambapo ndipo zilipo ofisi za kata, Bw. Athumani Makuka amekiri kuwachukulia hatua wale wote wasiozingatia kanuni na taratibu zilizowekwa katika kutimiza adhma ya kuliweka Jiji katika Hali ya usafi muda wote.
"Ushiriki wa wananchi ni mzuri na unatia moyo tangu tulipoanza masuala ya usafi na tumekuwa tukiwaomba Taasisi mbalimbali za mazingira kushirikiana na sisi na wamekuwa wakituunga mkono katika kulitekeleza hili.

"Tunawachukulia Sheria wale wote wasio hudhuria siku ya usafi ambayo ni jumamosi ikiwa ni kutozwa faini na kufikishwa kwenye Ofisi ya Mtendaji wa kata na tunashirikiana na polisi jamii katika kulitekeleza agizo hili la usafi wa mazingira na kuliweka Jiji letu katika Hali ya usafi,"amesema Makeka

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news