Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) wafanya mkutano wa bodi

NA FRESHA KINASA

SHIRIKA la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na mapambano ya ukatili wa kijinsia katika Mkoa wa Mara limefanya mkutano wa bodi wa shirika hilo na kujadili mambo mbalimbali yanayolenga kuendeleza mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni na aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia.
Mkutano huo umefanyika Februari 28, 2023 makao makuu ya shirika hilo yaliyopo Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara na kuongozwa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika hilo, Steven Kolokoni pamoja na Mkurugenzi wa shirika hilo,Rhobi Samwelly.
Akizungumza na DIRAMAKINI Mkurugenzi wa shirika hilo,Rhobi Samwelly amesema mkutano huo ulijadili mikakati mbalimbali ikiwemo kuendelea kutoa elimu katika jamii ya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji na ndoa za utotoni, kutoa hifadhi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kupitia kituo cha Hope Mugumu Nyumba salama na Nyumba Salama Butiama.
Pia, amesema kuwaendeleza watoto wa kike kielimu na kifani ili wafikie ndoto zao. kuendelea kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa wahanga wa ukatili wa Kijinsia sambamba na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake kusudi waweze kujikwamua kiuchumi.
Aidha, Rhobi amewasihi wananchi kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwani vitendo hivyo ni kinyume cha sheria za nchi na haki za binadamu na kwamba mapambano hayo yanahitaji ushirikiano wa pamoja baina ya wananchi, serikali na wadau.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news