Serikali kulipa fidia wananchi wa Mianzini jijini Arusha kupisha ujenzi barabara kilomita 18

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imeahidi kulipa fidia kwa wananchi wa maeneo ya Mianzini wanaopitiwa na ujenzi wa barabara ya Olemringaringa - Ngaramtoni Juu yenye urefu wa kilometa 8.5 inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
Kazi za ujenzi wa barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) kwa kiwango cha lami zikiendelea mkoani Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 23 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2023.
 
“Sehemu ambazo barabara imefuata wananchi, tutawalipa mara baada ya zoezi la tathmini linaloendelea kukamilika kwani ni haki yao,”amesema Prof. Mbarawa.

Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni ahadi iliyotolewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati. Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kujengwa kwa kiwango cha lami na unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja na utatekelezwa kwa muda wa miezi 15 ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti, 2023.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati akikagua hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) ambao ujenzi wake umefikia asilimia 23, mkoani Arusha. Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

“Serikali hii ni sikivu na inaendelea kutekeleza ahadi zilizotolewa na Serikali za Awamu zilizopita ili kuendelea kuboresha hali ya miundombinu nchini na kufungua mawasiliano hususani katika miundombinu ya barabara,”amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ametoa wito kwa Meneja wa Mkoa wa TANROADS kusimamia ujenzi wa barabara hiyo na kuhakikisha thamani ya fedha na ubora wa barabara unaonekana pale ujenzi utakapokamilika.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Steven Zelothe, akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati Waziri huyo akikagua ujenzi wa barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) kwa kiwango cha lami mkoani Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 23 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2023.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Steven Zelothe, amempongeza Mhe. Rais wa Awamu ya Sita kwa kuwa wananchi wanaendelea kuona juhudi za dhati zinazoendelea kufanywa na Serikali hii hasa kwa mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa haraka wa wakazi wa maeneo hayo na kuongeza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Arusha, Eng. Reginald Massawe, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa pamoja na uongozi wa mkoa wakati wakikagua barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) kwa kiwango cha lami ambao ujenzi wake umefikia asilimia 23, 2023.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Eng. Reginald Massawe, ameeleza kuwa barabara hiyo imesanifiwa kubeba ekseli za magari zipatazo milioni 3 zenye uzito wa tani 8 kila moja katika muda wa miaka 20.

Amesema kuwa hadi sasa mkandarasi amekwishaleta mitambo, vifaa na magari yanayotumika kwenye kazi za ujenzi wa barabara hiyo na matumaini yao mradi utakamilika kama ulivyopangwa.
Kazi za ujenzi wa barabara ya Mianzini - Olemringa - Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha – Timbolo (Km 18) kwa kiwango cha lami zikiendelea mkoani Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 23 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2023.

Ujenzi wa wa barabara ya Mianzini – Olemringaringa – Ngaramtoni Juu na Olemringaringa - Sambasha/Timbolo (Km 18) unatekelezwa na mkandarasi kutoka kampuni ya STECOL Corporation kutoka China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 22.22.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news