Mambo saba ya kumtambua mtumishi au kanisa la uongo linalotaja jina la Yesu

[1]. Wanataja jina la YESU ila huwa hawataji sana HESHIMA ya vyeo vyake kama, BWANA YESU, YESU KRISTO, YESU MWANA WA MUNGU, YESU MWOKOZI.

Huwa mara nyingi wanataja jina la Yesu bila vyeo vyake

[2]. Huwa hawaongelei sana dhambi Wala kuhamasisha Toba ya dhati Kwa mtenda dhambi au kukemea dhambi kwa watu hii ni kwa sababu nguvu za shetani wanayemtumikia ni dhambi za watu Kwa hiyo wakikemea dhambi au kuhamasisha toba Wanammaliza shetani mungu wao nguvu.

[3].Huwa hawasisitizi WOKOVU na UBATIZO

Hawa Huwa hawaongelei kabisa kuokoka Wala kubatizwa, na wakiamua kubatiza hubatiza tofauti na Yesu na mitume( HAWABATIZI Kwa kuzamisha majini na Kwa jina la Yesu). Hii ni Kwa sababu wanajua MTU asipobatizwa HAWEZI kuwa Mkristo.

[4].Huwa hawamsemi, hawamsisitizi Wala kumtegemea ROHO MTAKATIFU

Hii ni Kwa sababu roho wanayoitumia Sio ya YESU KRISTO MWANA WA MUNGU, Kwa hiyo ROHO MTAKATIFU kwao hausiki kufanya miujiza, KUFUNDISHA, kuponya Wala KUTOA unabii, na pia wanajua Ukiwa na Roho MTAKATIFU utajua wanachokifanya kuwa ni Uongo.

[5].Mahubiri Yao mengi yanahusu mada tatu tu yaani UTAJIRI, UPONYAJI, MIUJIZA

Hii ni Kwa sababu hizi ndo ajenda za shetani KUPOTEZA watu kutoka kwenye mafundisho ya Yesu aliyofundisha ya HAKI, TUMAINI NA UPENDO.

[6].Wanasisitiza sana watu kutoa SADAKA

Hii ni kwa sababu mojawapo ya malengo yao ya kutafuta hizo nguvu na kuanza hiyo kazi ni wao kupata UTAJIRI na fahari ya Dunia na kuwa maarufu duniani.

[7].Maisha Yao Huwa hayana ushuhuda wa utakatifu

Mara kadhaa utawakuta wakiwa na skendo za kufanya dhambi japo Huwa HAMNA ushahidi WA wazi Kwa sababu Huwa wanalindwa na kutetewa.

UKIONA JAMBO MOJAWAPO KATI YA HAYO JUA UKO KWENYE MTEGO WA SHETANI

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news