Mtwara-Mikindani yazindua Wiki ya Mwanamke

NA DIRAMAKINI

KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani ,Wanawake wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani mkoani Mtwara wakiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Rizex Foundation, Bi. Riziki Ahmedi Abbass aliyeambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mhe. Shadida wamefanya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mwanamke kwa kukabidhi vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa na wagonjwa waliolazwa kwenye wodi ya akina mama katika Kituo cha Afya cha Likombe.
Mkurugenzi huyo pia amekabidhi vifaa vya kupimia saratani ya matiti na shingo ya kizazi kwa madaktari wanawake wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani ambavyo watavitumia kwenye zoezi la upimaji wa magonjwa hayo kuanzia leo Machi 2 hadi 8, mwaka huu katika viwanja vya Mashujaa.
Katika wiki ya maadhimisho ya siku ya mwanamke Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepanga kufanya matukio mbalimbali ikiwemo ugawaji wa mashuka Kituo cha Afya Mikindani, kupata chakula na wazee wanawake, kufanya mdahalo wa masuala ya malezi na ukatili wa kijinsia, upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti bure pamoja na matukio mengine mengi.
Aidha Manispaa ya Mtwara-mikindani itaadhimisha siku ya mwanamke Duniani tarehe 7, Machi 2023 katika Viwanja vya Mashujaa huku kimkoa yakiadhimishwa Wilaya ya Tandahimba tarehe 8, Machi 2023 yakiwa na Kauli Mbiu inayosema “ Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news