Mambo ya kuzingatia unapokuwa mgeni nyumbani kwa watu

NA MWANDISHI WETU

NI wazi kuwa, mgeni anapokuwa mahali ambapo ni ugenini kama tulivyo sisi hapa duniani, huwa ni mwenye kujifunza yale yaliyopo mbele yake. 

Mgeni kwa asili yake huwa ni mwenye fikra huru (open-minded) ya kupokeya yale mapya atakayoona ugenini. Haya hapa mambo ya kuzingatia;
Picha na Freepik.

1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGODOGO

Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya mswaki, taulo na mahitaji yako mengine madogomadogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...kwa wenyeji sio vizuri.

2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI

Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.

3. USIBAKI SEBULENI

Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA

Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

5. USIINGILIE MAZUNGUMZO

Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.

6. USITEMBELEE MAJIRANI

Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.

7. KULA VYAKULA VILIVYOPO

Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.

8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI

Usianze kutumia vifaa vya wenyeji kama vyako.

Ukizingatia haya utaishi kwa watu mda mrefu.Tuwe na heshima tunapokuwa ugenini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news