Kamati ya Bunge yapitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mwaka 2023/24

NA MWANDISHI WETU

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Kikao cha kamati hiyo kimefanyika Machi 22, 2023 chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameiongoza Menejimenti ya Ofisi hiyo kuwasilisha mpango na bajeti ya ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, Bungeni, Jijini Dodoma,tarehe 22 Machi, 2023.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq akifuatilia taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2023/24 wakati wa kikao hicho kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma Machi 22, 2022. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Rehema Kipera. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akichangia jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq akieleza jambo wakati wa kikao hicho.Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma, Machi 22, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akichangia jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Mariam Kisangi akichangia hoja wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma,Machi 22, 2022.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na menejimenti ya ofisi hiyo Bungeni, Jijini Dodoma, Machi 22, 2022.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news