Msajili Mkuu akagua eneo la ujenzi Mahakama Kuu Geita

NA CHARLES NGUSA

MSAJILI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma hivi karibuni alifanya ziara katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita kwa lengo la kukagua eneo linalopendekezwa kujengwa Mahakama Kuu katika Mkoa wa Geita.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akiteta jambo na viongozi katika ziara yake.
 
Katika ziara hiyo, Mhe Chuma aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza, Mhe. Chiganga Tengwa na kupokelewa na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita na Mahakimu ya Wilaya Geita.

Baada ya kupata taarifa za awali, Msajili Mkuu aliendelea na ziara yake ya kukagua eneo hilo ili kuona kama lina sifa zinazohitajika na miundombinu iliyopo.

Kadhalika, Mhe. Chuma alitembelea jengo la Mahakama ya Mwanzo Nyankumbu ambalo litatumiwa kwa muda na Mahakama ya Hakimu Mkazi. Pia alikagua eneo lililokuwa likitumiwa na Halmashauri ya Wilaya Geita, ambapo Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Geita zitahamia hapo katika zoezi zima la kupisha ujenzi wa Mahakama Kuu.

Akiongea na watumishi baada ya kutembelea maeneo hayo, Msajili Mkuu aliwahimiza viongozi walioshiriki mafunzo ya mfumo mpya wa usimamizi wa mashauri (advanced case management) kuwafundisha maafisa wa Mahakama kwa kuwa wao ndiyo watakuwa watumiaji wa mfumo huko kwa asilimia kubwa. Mhe. Chuma pia alihimiza watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na bidii. Naye Naibu Msajili aliahidi kutoa elimu aliyoipata kwa walengwa wote

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news