Mwili wa aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (1995-1996) Martine K. Mbago waagwa kijeshi

NA DIRAMAKINI 

KAMISHNA wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza akimwakilisha Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Machi 6, 2023 ameungana na Waombolezaji katika Misa ya Kuuaga Kijeshi Mwili wa aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (1995-1996), Martine K. Mbago nyumbani kwa marehemu Chanika Zingiziwa nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu za rambirambi, Kamishna Semwanza alisema Marehemu Kamishna Mstaafu Mbago, alitumikia vyema na ni miongoni wa Waanzilishi ambao wamelitengeneza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuwa na mwonekano tunaouona leo.

Pia aliongeza kuwa, marehemu alifanya kazi kwa uaminifu na kwa weledi na kuwatengeneza Maafisa na Askari ili kuja kulitumikia Jeshi katika Huduma za Kuzima Moto na Uokoaji.
"Kwa ujumla,marehemu alifanya kazi kwa weledi, uaminifu na uadilifu, amewatengeneza Askari na Maafisa ili kuja kulitumikia Jeshi na Taifa kwa ujumla katika huduma za Kuzima Moto na Uokoaji katika dharura mbalimbali,"alisema Kamishna Semwanza.
Katika misa hiyo ya kuuaga mwili wa Kamishna Mbago, viongozi mbalimbali walihudhuria ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Benard Mchomvu, Makamishna Wastaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara na Kamishna Mstaafu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Ali Malimusy.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa shukurani za dhati kwa wote waliohusika katika kufanikisha zoezi la mazishi ya mwili wa marehemu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news