NAIBU WAZIRI PINDA AITAKA OFISI YA KAMISHNA WA ARDHI TANGA KUONGEZA KASI YA UPIMAJI ARDHI

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geofrey Pinda ameitaka ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tanga na halmashauri zake kuongeza kasi ya upimaji ardhi katika maeneo mbalimbali ili kuepuka uvamizi wa maeneo ya watu na maeneo ya hifadhi.
Ametoa kauli hiyo Machi 7, 2023 wakati akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria kikao cha siku moja wilayani Handeni, mkoani Tanga wakati wa kukabidhi rasmi mradi wa makazi maalum katika kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi.

"Kamishna wa Ardhi mkoa wa Tanga jitahidi usimamie upimaji wa ardhi wa mkoa huu mkoa usingekuwa na matatizo yoyote ya ardhi kama tungepima haya maeneo, sehemu kubwa kwasababu tuna zembea mpaka wananchi wanaenda wanavamia halafu ndio tunataka sasa kuwaondoa kwa vurugu," alisema Mhe. Pinda.
Katika kutilia mkazo suala hilo,Mhe. Pinda aliwashauri viongozi wa Halmashauri kuepuka kuingia kwenye maeneo ambayo yamekatazwa kabla kuingia kwenye mazungumzo kuhusu umiliki wa eneo husika kwa sababu inawachanganya kwenye maamuzi.

Kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni kwa sasa ni makazi ya wananchi ambao kuanzia Juni, 2022 walihama kwa hiyari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro ili kulinda ikolojia na uoto wa asili katika eneo hilo. Mara baada ya kuwasili, walipewa nyumba za kuishi za ukubwa wa vyumba vitatu kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 2.5 na jingine la malisho la ekari tano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news