Ni Clatous Chama na Sadio Kanoute

NA DIRAMAKINI

NYOTA wawili wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Nyota hao ni Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao wanaowania tuzo hiyo pamoja na Mahmoud Kahraba na Pecy Tau wote kutoka Al Ahly.

Katika mchezo wa Simba uliopita dhidi ya Horoya walioibuka na ushindi wa mabao 7-0, Chama alifunga mabao matatu ‘hat trick’ akisaidia kupatikana kwa jingine moja wakati Kanoute akitupia mawili.

Zoezi la mashabiki kupiga kura linaendelea katika ukurasa rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.Chama ndiye aliibuka mchezaji bora wa CAF wiki iliyopita na sasa anawania tena nafasi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news