Rais al Sisi atoa onyo kali kwa Wamisri

CAIRO-Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri ameonya kuhusu matokeo hasi dhidi ya maandamano yoyote yatakayofanywa kulalamikia hali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini humo.

Picha ya maktaba ikimuonesha Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi akitoa hotuba wakati wa sherehe za mahafali katika Chuo cha Kijeshi cha Misri mjini Cairo hivi karibuni. (Picha na AFP).

Pia amewatahadharisha Wamisri kutorejelea kile kilichotokea kabla, wakati na baada ya maasi ya Januari 25, 2011, ambayo yaliondoa utawala wa Hosni Mubarak.

Akihutubia hadhara kubwa iliyojumuisha maafisa wa jeshi na polisi, makasisi, wanahabari na viongozi wa Bunge,Alhamisi ya wiki hii, Rais Sisi alisema: "Wamisri wanapaswa kujihadhari na kusababisha uharibifu wa nchi yao tena.Kuharibu nchi kutoka ndani ni jambo hatari zaidi kulifanya."

Wataalamu wanasema maonyo ya utawala huo juu ya hatari ya ukosefu wa usalama na ukosefu wa utulivu yana uwezekano wa kuongeza zaidi ya wasiwasi ulioenea juu ya kuzorota kwa hali ya maisha, hata kama Wamisri wengi wanathamini juhudi za serikali za kurudisha itikadi kali na kuzuia tishio la ugaidi.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Misri, Amr Mouss alitoa angalizo kwamba kuna hali ya wasiwasi, ya kukatisha tamaa na kupoteza matumaini inayotawala nchini Misri, hivyo kuna udharura wa hali hiyo kuponywa mara moja.

Februari,mwaka huu wabunge wa Bunge la Misri, nao pia walionya juu ya ugali wa bei za vitu na kuadimika kwa bidhaa za msingi na kukatishwa tamaa wananchi na wakaituhumu serikali kwamba imeshindwa kukabiliana na mfumuko wa bei uliokithiri, upandishwaji mkubwa wa bei za bidhaa na kuadimika bidhaa za msingi.

Pia, wachumi wanafafanua kuwa, hali mbaya ya uchumi wa Misri haijakomea kwenye madeni tu iliyonayo nchi hiyo, kwani mfumuko wa bei unaoongezeka mwezi baada ya mwezi na kushuka thamani ya sarafu ya pauni.

Wakati huo huo, uwekezaji wa kigeni unashuka kwa kiwango kikubwa huku mapato yatokanayo na utalii na fedha zinazotumwa na Wamisri wanaofanya kazi za vibarua nje ya nchi, ambavyo ndivyo vyanzo viwili vikuu vya fedha za kigeni kwa nchi hiyo zikiwa zimepungua.

Kiongozi wa zamani wa Chama cha Al Karama, Muhammad Sami alisema huenda hoja zinazotumika kuwazuia watu kuingia mitaani zisiwe na mashiko, kwani mwananchi wa kawaida ana vigezo tofauti na wanasiasa na watoa maamuzi, kwani ana nia zaidi ya kupata mtu anayestahili kumuwezesha kuishi kuliko kuhusu masimulizi ya kihistoria juu ya hasara za maandamano.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais al Sisi kuelezea mashaka yake juu ya athari mbaya za uasi wa Januari 2011, akielezea tukio hilo kama chanzo cha uharibifu wa nchi na karibu kuanguka kwa serikali, kama sio jeshi kuingilia kati kwa nguvu, kuweka utulivu na kuwafukuza wanamgambo wenye silaha katika Peninsula ya Sinai mambo yangeharibika.

Rais al Sisi alisisitiza jambo hilo huku akisisitiza kuwa, mgogoro wa kiuchumi sio kipimo cha haki cha mafanikio ya serikali hadi sasa.

Bila kujali matokeo ya maonyo ya Rais al Sisi juu ya athari mbaya za machafuko ya ndani, wachambuzi wanasema, mamlaka za Misri zinaonekana kufahamu kikamilifu kwamba nchi inakabiliwa na matarajio ya wazi ya uasi wa tatu, kwa sababu makundi makubwa ya wakazi wana hasira juu ya hali yao na wanaweza kujisikia hawana cha kupoteza kwa kuonyesha hasira na kutoridhika kwao.(Mashirika)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news