Rais Dkt.Mwinyi atunukiwa tuzo ya Kimataifa ya 'VIP Global Water Changemakers Awards'

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Tuzo Maalum ijulikanayo kama VIP Global Water Changemakers Awards kutokana na jitihada zake za kuifanya Zanzibar kuwa wa kwanza barani Afrika kuanzisha na kuzindua programu ya uwekezaji katika Sekta ya Maji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hilary, tuzo hiyo imetolewa Machi 22, 2023 pembezoni mwa Mkutano wa Maji wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Lengo likiwa ni kutambua na kuthamini mchango wa viongozi kupitia uwekezaji kwenye Sekta ya Maji katika nchi zao.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi katika hafla hiyo amewakilishwa na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dkt.Suleiman Haji Suleiman jijini humo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akionesha Kitabu cha Mpango wa Miaka Mitano ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji Zanzibar, baada ya kuzindua mpango huo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Sekta ya Maji barani Afrika, uliofanyika Machi 11, 2022 katika Ukumbi wa Hoteli ya Melia Kiwengwa na kulia kwa Rais ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya GWPSA),Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar, Mhe.Shaib Hassan Kaduara.(Picha na Maktaba/ Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news