Rais Dkt.Samia afanya mabadiliko ya makatibu tawala, amteua Kamishna wa DCEA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Makatibu Tawala wa Mikoa katika mikoa mitatu na Makatibu Tawala wengine watatu kuhamishwa vituo vya kazi na kupelekwa mikoa mingine.
Pia, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amemteua Aretas James Lyimo kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA), ambaye anachukua nafasi ya Gerald Kusaya ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ameeleza leo Machi 16,2023 kuwa, miongoni mwa makatibu tawala wa mikoa walioteuliwa ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Ally Gugu ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara,Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda anachukua nafasi ya Willy Machumu ambaye amestaafu.

Mheshimiwa Rais pia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,Kusaya ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.

Kwa upande wa Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo ni pamoja na Dkt. Fatuma Mganga ambaye amehamishwa kutoka Mkoa wa Dodoma kwenda Mkoa wa Singida,Dkt.Maganga anachukua nafasi ya Dorothy Mwaluko ambaye amestaafu.

Rais Dkt. Samia amemuhamisha Rashid Mchata kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda Mkoa wa Pwani ,Mchata anachukua nafasi ya Zuwena Omary ambaye amehamishiwa Mkoa wa Lindi na Zuwena amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda Mkoa wa Lindi,Zuwena anachukua nafasi ya Ngussa Samike ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news