Serikali yapiga marufuku huduma za bweni kwa wanafunzi awa awali hadi darasa la nne

NA DIRAMAKINI

KAMISHNA wa Elimu Tanzania, Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema ni marufuku kwa shule yoyote kutoa huduma ya bweni kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne isipokuwa kwa kibali maalum tu ambacho kitatolewa na Kamishna wa Elimu.

Kupitia Waraka wa Elimu namba 2 wa mwaka 2023 ulitolewa na Kamishna huyo, shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa hayo yasiyoruhusiwa zimeagizwa kusitisha huduma iyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka huu 2023. “Huduma za bweni zitolewe kuanzia darasa la tano na kuendelea.

“Malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi au walezi wa watoto hao, imebainika kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi darasa la nne.

“Huduma za bweni kwa wanafunzi wenye umri mdogo ikiwemo wale wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne huwanyima watoto fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendelo ya familia na jamii zao, kulingana na tafiti zilizopo, madhara ya muda mrefu yatokanayo na tabia ya kulaza watoto bweni katika umri mdogo ni watoto kukosa mapenzi kwa wazazi,walezi na jamii zao na hivyo kushindwa kuwa sehemu ya familia na jamii husika” ameeleza Kamishna wa Elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news