Yanga SC yafunga na kufungua faili la Feisal Salum Abdallah, yatoa amri

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga imeutaarifu umma kuwa imepokea maamuzi ya marejeo ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kuhusu suala la mchezaji wake Feisal Salum Abdallah.
Baada ya kupokea maamuzi hayo, Klabu ya Yanga imemwandikia barua Feisal Salum kumtaka aripoti kambini haraka iwezekanavyo na kuendelea kuutumikia mkataba wake kama mchezaji halali wa Yanga mpaka tarehe 30, Mei 2024, kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.

Aidha, Klabu ya Yanga iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezaji wake wanaofanya vizuri, Uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum Abdallah na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake, kama wataridhia.

Mwisho, Klabu ya Yanga inapenda kuutaarifu umma kwamba iko tayari kumruhusu Feisal Salum Abdallah kuondoka klabuni kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa wachezaji zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA. 

Ikiwa pia kuna klabu yoyote inahitaji huduma ya mchezaji huyu, klabu ya Yanga iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news