SERIKALI YASEMA UJENZI NA UKARABATI WA VIVUKO KUTATUA CHANGAMOTO YA USAFIRI KANDA YA ZIWA

NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kuwa kukamilika kwa ujenzi wa vivuko vipya vinne na ukarabati wa vivuko vinne vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria kutapunguza changamoto za usafiri kwa wananchi wanaoishi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kutarahisisha shughuli za maisha kwa urahisi, uhakika na usalama.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Songoro, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, kuhusu ujenzi wa vivuko vipya vinne, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Hayo yamesemwa mkoani Mwanza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua karakana ya ujenzi wa meli na vivuko ya Songoro na kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa vivuko hivyo vitavyogharimu takribani bilioni 26 na kutarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi Eng. Aloyce Ndunguru, wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya vivuko vipya na matengenezo ya vivuko katika yard ya Songoro Marine, mkoani Mwanza.

“Nimekagua na nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vivuko vipya lakini pia na ukarabati wa vivuko unaoendelea, nimatumaini yangu vivuko hivi vitakamilika ndani ya muda kwani kuna baadhi ya maeneo vivuko hivyo havipo au kimebakia kimoja na hivyo kutokidhi mahitaji ya wananchi,"amesema Kasekenya.
Muonekano wa awali wa sehemu ya vivuko vinne vinavyojengwa na Kampuni ya Songoro Marine, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Amefafanua kuwa, kwa sasa ujenzi wa vivuko hivyo unaendelea na vipo katika hatua mbalimbali na kutaja kuwa vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Aidha, ukarabati wa vivuko unaoendelea ni pamoja na MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akikagua baadhi ya vipuli vitavyofungwa katika vivuko vinne vinavyofanyiwa matengenezo/ukarabati katika yard ya Songoro, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).

Aidha, ameiagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kumsimamia mkandarasi wa Kampuni ya Songoro kufunga vifaa vyote vilivyosanifiwa kuanzia katika hatua za awali hadi vivuko hivyo vitapokamilika.
Muonekano wa Kivuko cha MV Misungwi kinachotoa huduma katika eneo la Kigongo na Busisi kikiwa katika matengezo katika yard ya Songoro, mkoani Mwanza.
Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi, Mhandisi Aloyce Ndunguru, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, kuhusu ujenzi wa vivuko vipya vinne, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Naye, Kaimu Meneja Vivuko Kanda ya Ziwa na Magharibi kutoka TEMESA, Mhandisi Aloyce Ndunguru, amesema kuwa wanaendelea na ujenzi wa vituo vipya vitatu ambvyo ni Bwiro (kisiwani) – Bukondo katika Wilaya ya Ukerewe, Kituo ch Ijinga (kisiwani) – Kahangala katika Wilaya ya Magu na Kituo cha Mayenzi – Kanyinya ambapo miradi hiyo ikikamilika itafanya wawe na jumla ya vituo 16 katika kanda hiyo.

Ameeleza pia kanda hiyo ina jumla ya vivuko 17 ambapo kati ya hivyo vivuko vinne vipo katika matengenezo makubwa ambavyo ni MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).
Muonekano wa awali wa sehemu ya vivuko vinne vinavyojengwa na Kampuni ya Songoro Marine, mkoani Mwanza. Vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Songoro, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baadhi ya vivuko ambavyo vinafanyiwa ukarabati vipo katika hatua za mwisho za kukalimika na vitarudishwa TEMESA mapema kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news