Watakiwa kuchangia fedha za chakula cha mchana kwa wanafunzi Kidato cha Pili na Nne

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAZAZI wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamehimizwa kuchangia chakula cha mchana shuleni kwa watoto wao walioko katika maradasa ya mitihani ili waweze kujiandaa vizuri katika mitihani ya kitaifa

Hayo yamesemwa katika matangazo ya misa ya Jumapili ya nne ya Kwaresma, Parokiani Chamwino Ikulu, katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma na Katibu wa Parokia hiyo Dkt. David Msimbe alipokuwa akisoma barua kutoka Serikali ya Kijiji cha Chamwino Ikulu ambayo iliwaomba wakazi wote wa eneo hilo kuhakisha kama wana watoto wao wanaosoma Shule ya Sekondari Chamwino kulipa pesa ya chakula cha mchana shuleni hapo mara moja kwa wanafunzi wa kidato cha Pili na cha Nne na kinyume chake Machi 23, 2023 wataanza kuwachukuliwa hatua kali.

“Jamani ninawaombeni mlipie haraka vyakula vya watoto wetu huko shuleni mapema sana, itakuwa ni fedhea na aibu kwetu kama kutakuwa na Mkatoliki siku ya Machi 23, 2023 akiwa ni miongoni mwao ambao hawajalipa pesa hiyo ya chakula,"alisisitiza Katibu huyo wa Parokia hiyo baada ya kumaliza kusoma barua kutoka Kijiji cha Chamwino Ikulu.

Mwandishi wa ripoti hii aliona umuhimu mkubwa wa chakula cha mchana shule za kutwa kutolewa kwa wanafunzi wote ili kuwaandaa vizuri wanafunzi wa kidato cha kwanza na tatu kabla ya kuwa madarasa ya mitihani.

Kiongozi huyo wa Parokia hii pia aliwakumbusha waumini wa Kanisa hilo kuwa Machi 17, 2021 ni siku aliyofariki dunia mwana parokia mwenzao Mheshimiwa John Pombe Magufuli na kwa heshima yake waamini hao walitumia dakika chache kumkumbuka.

“Tunamkumbuka kwa kuwa aliweza kufanya mambo mengi makubwa ya maendeleo kwa muda mchache aliyokuwepo hapa duniani.”

Awali katika mahubiri ya Misa hiyo Padri Paul Mapalala ambaye pia ni Paroko alisema kuwa Wakristo wanatakiwa kuondoa upofu wao na kumuona Mungu katika Kipindi cha Kwaresma kwa kila mmoja kumfikiria mwenzake mazuri na kuacha kusontana vidole.

“Sisi sote ni vipofu wa kwenda mbinguni na wa kumuona Mungu, si vipofu kwa maana tunashindwa kuona hapana ni vipofu kwa kuwa hatumjui Mungu. Kama unasema unampenda Mungu usiyemuona unamchukiaje unayemuona ! Mbona haumtendei vizuri?”

Mara baada ya mahubiri haya ya misa hiyo ulifika wakati wa maombi na mojawapo lilikuwa hili,“Utufungue macho yetu, tuone shida za wenzetu na kuwasaidia.”

Hadi misa hiyo ya kwanza inamalizika hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu ilikuwa ya jua la kadili huku baadhi ya wakulima ambao walipanda mahindi ya mbegu za muda mfupi wakianza kuchemsha na kuchoma mahindi hayo majumbani mwao.Mandhari ya mshimo ya takataka yakionekana majani na mabunzi ya mahindi yaliyochomwa na kuchemshwa. Hata mitaani mtu anapozunguka anaona vijana wanaouza mahindi ya kuchoma wakiongezeka katika eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news