Daktari afunguka madai ya dawa za meno, miswaki kuhusishwa na ushoga

NA DR.BARAKA NZOBO

KUMEKUWA na sintofahamu inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya maeneo ya jamii kuhusu dawa za meno, miswaki na vipeperushi vya uboreshaji wa Afya ya Kinywa na Meno kuhusishwa na masuala ya ushoga na usagaji. 

Viambata (ingredients) vilivyomo kwenye dawa za meno za kupigia mswaki kwa ajili ya kulinda Afya ya Kinywa na Meno kwa ujumla ni hivi vifuatavyo (Angalia boksi au tube ya dawa yako ya meno): 

Sodium lauryl sulfate (SLS), cocamidopropyl betaine and sodium methyl cocoyl taurate (adinol),calcium carbonate, calcium phosphate salts, alumina, silica, and magnesium carbonate, carrageenan, spearmint or peppermint, xylitol, sucralose, or sodium saccharin, glycerol and sorbitol , include trisodium phosphate, sodium citrate, sodium hydroxide and pyrophosphates; titanium dioxide , sodium monofluorophosphate (MFP), sodium fluoride (NaF) and stannous fluoride (SnF2) na Hydroxyapatite.

Hakuna kiambata hata kimoja chenye uwezo kuingia na kuharibu mfumo wa vichocheo vya uzazi (reproductive hormones) vya mwanamke au mwanaume. Pia hakuna kiambata hata kimoja chenye uwezo wa kuingia kwenye mfumo wa vinasaba (DNA) wa binadamu.

Kwahiyo uzushi unaendelea kwenye mitandao ya kijamii upuuzwe maana ni upotoshaji wa hali ya juu. 

Wananchi wanasisitizwa kuendelea kupiga mswaki meno yao ili kujikinga na tatizo la ugonjwa wa kuoza meno unaoathiri idadi kubwa ya watanzania.

Dawa za Meno za Kupigia Mswaki ni salama kwa matumizi ya mwanadamu kujikinga na Magonjwa ya Fizi na ya Kuoza kwa Meno.

Ushoga au Usagaji ni tabia ya mtu aliyojifunza anakokujua yeye; watu wasitafute vichaka vya kujifichia kuhalalisha tabia zao mbaya mbele ya wanadamu na Mwenyezi MUNGU.

Mwandishi ni Dkt.Baraka Nzobo
DDS, MSc Tropical Disease Control
(0655749355)
bnzobo@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news