Haji Manara amuuma sikio Nandy

NA DIRAMAKINI

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amemtaka nyota wa muziki Tanzania,Faustina Charles Mfinanga (Nandy) kutambua kuwa, ukiwa mtu maarufu kusemwa ni jambo la kawaida.

"Nandy mdogo wangu,shemeji wangu na rafiki yangu jana umeniangusha sana na sitegemei urudie tena kulalamika na kulia kisa umesemwa.

"Utaachaje kusemwa wakati wewe ni Super Star? Nani alikuwa anakusema ulipokuwa kwenu Upareni Sijui uchagani, unasemwakKwa kuwa wewe ni maarufu na celebrity, unasemwa kwa kuwa ni Nandy na sio Nandela,otherwise ungebaki kijijini uchemshe viazi kama utasemwa na mtu.

"Unasemwa kwa kuwa una kitu, ungetaka usisemwe ungebaki raia wa kawaida mtaani, us longer as umechagua maisha uliyonayo sasa lazima usemwe utake usitake, na waja hawapangiwi la kusema,waache ni haki yao kwa sababu wewe ni Nandy.

"Diamond Platnumz kasemwe mangapi, kafa? Kaathirika na nini zaidi ya kukuza jina lake na kuendelea kuwa Star? Amesemwa hadi na aliowasaidia na kuwapa maisha, kimepungua nini kwake?.

"Wewe unasemwa kuliko mimi? Lipo kundi likilala likiamka ni Haji tu, wamenipunguzia nini zaidi ya kuonyesha How HAJI is BIG?.Yupo dada anajiita wa Taifa, ishapita wiki bila kuandika jambo kuhusu mimi?.

"Mara nimechafua hali ya hewa mara nimempiga mke wangu,mara mimi muhuni nakaza hovyo mademu, kapata nini? Nini kimeniathiri katika porojo zake za kutafuta rizki? Sanasana anakuza my brand.

"Wenzio hata tukipost Ijumaa Kareem au Eid Mubarak tunasemwa, hata hii post yako niliokushauri kwa nia njema kuna kuku watanisema.

"Unawezaje kuchukuia kusemwa au kuwapangia Walimwengu matumizi ya mdomo wao? Tumechagua wenyewe life hizi za umaarufu,hatuna haki ya kuwazuia midomo yao,tena haifai kuwalazimisha watuseme kwa mazuri tu,,waacheni waseme na waseme na waseme,si tumetaka wenyewe kuwa brand?.

"Juzi ulisemwa kuhusu handbag yako, ukajbu vizuri kabisa nani alionekana mjinga baina yako na dada feki wa Taifa alikokimbia?.Yes, mengine yajibu, lakini mengi potezea na hiyo ndio raha na karaha ya kuwa maarufu na star inauma, lakini tustahmili tu.Hope next time ukisemwa tena utafanya na Party ya kufurahia ukubwa wako,hapana kulia na usihuzunike,"Haji Manara amemshauri Nandy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news