Jaji Komba atoa wito kwa watumishi wa Mahakama wilayani Bunda

NA FRANCISCA SWAI

JAJI wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba wamewaasa watumishi wa Mahakama Wilaya ya Bunda kufanya kazi kwa bidii licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Marlin Komba (wa tatu kushoto) akikagua mazingira nago la Mahakama ya Wilaya Bunda.

Mhe. Komba alitoa rai hiyo hivi karibuni katika ziara aliyoifanya akiwa ameambatana na Naibu Msajili wa Kanda hiyo, Mhe. Frank Moshi na Mtendaji wa Mahakama Musoma, Bw. Festo Chonya kukagua shughuli mbalimbali za kimahakama ndani ya Wilaya hiyo.

Viongozi hao walibaini baadhi ya Mahakama kama Mahakama ya Mwanzo Mcharo na Mahakama ya Mwanzo Mugeta zipo katika majengo ya ofisi za Kata, jambo ambalo huleta mwingiliano wa shughuli za kimahakama na Serikali.

Wakiwa katika Mahakama ya Mwanzo Nansimo, viongozi hao walipongeza jitihada na ubunifu wa kuboresha mazingira ya kazi inayofanywa na Hakimu Mkazi, Mhe. Chana Chana na kumshukuru kwa kuziona changamoto na kuzifanya fursa, hatua ambayo itaacha alama ya utendaji kazi wake mzuri.

Aidha, viongozi hao wamesisitiza kufanya kazi kwa umoja na upendo, kuhakikisha mapato ya Serikali hayapotei, kusikiliza mashauri na kutolea maamuzi kwa wakati. Waliwaasa Mahakimu kuhakikisha hawazalishi mahabusu isipokuwa kwa sababu zisizozuilika.

Akiwa katika Mahakama hiyo, Jaji Komba na msafara wake alipokea pongezi kutoka kwa watumishi kwa ukarabati mkubwa uliofanyika katika jengo la Mahakama, jambo ambalo limewawezesha kutoa huduma katika jengo zuri. Pongezi kama hizo pia zilitolewa na watumishi baada ya viongozi hao kutembelea na kukagua Mahakama ya Mwanzo Kenkombyo. Katika ziara yake, Jaji Komba pia alitembelea Mahakama za Ikizu, Kabasa, Bunda Mjini na kumalizia katika Mahakama ya Wilaya Bunda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news