Makamu wa Rais asisitiza maadili mema kwa Watanzania

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo Aprili 12, 2023 wameungana na waumini wengine katika kushiriki Ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco Nzavery -Nyakahoja Jijini Mwanza. Ibada iliyoongozwa na Padre Victor Awiti.
Akiwasalimu waumini mara baada ya ibada hiyo, Makamu wa Rais amewasihi Wakristo na Watanzania kwa ujumla kujitafakari tena katika namna ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili. 

Amesema, mfumo mzima wa maadili kuharibika umepelekea ubadhirifu wa fedha za umma hivyo ni vema kuendelea kulinda maadili mema ya kitanzania kwa kuwapa miongozo watoto na kufuatilia mienendo yao wakati wote.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya kawaida ya asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco Nzavery -Nyakahoja jijini Mwanza leo Aprili 12, 2023.

Aidha, Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa pamoja na viongozi wa Serikali ili waweze kuongoza vema taifa kwa hekima ya Mungu.
Makamu wa Rais yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news