Makamu wa Rais:Watanzania acheni kutupa taka ovyo barabarani

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kuacha tabia ya kutupa taka ovyo katika maeneo mbalimbali wanayotumia hususani barabarani.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akiwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliopo Swaswa Jijini Dodoma mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo leo Aprili 16, 2023. 

Amesema uwepo wa mvua zisizotabirika ni kutokana na uharibifu wa mazingira uliokwishafanyika hivyo kila mmoja aone umuhimu wa utunzaji mazingira mazuri ambayo nchi imejaaliwa na Mwenyezi Mungu.
Makamu wa Rais ametoa rai kwa waumini hao na watanzania kwa ujumla kuona umuhimu wa kupanda miti katika makazi yao ikiwemo miti ya matunda na kivuli pamoja na kuongeza jitihada katika usafi wa mazingira ili kukabiliana na athari zitokanazo na uharibufu wa mazingira zinazojitokeza hivi sasa.
Halikadhalika Makamu wa Rais amewakumbusha waumini juu ya kuzingatia maadili mema ya kitanzania katika malezi ya watoto na vijana pamoja na kutoa wito kwa wamiliki wa taasisi za kutolea elimu kujielekeza katika kusimamia maadili mema ya kitanzania katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news