Nabii Dkt.Mjuni awamegea siri watumishi wa Mungu

NA DIRAMAKINI

MTUMISHI wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha amesema,watumishi wengi wa Mungu waliopiga hatua katika huduma na kueneza Upako wa Roho Mtakatifu ni kutokana na mchango mkubwa wa wake zao kuwaombea na wao kusimama imara katika maombi, kujiamini na uaminifu.

Upako wa Roho Mtakatifu ni uwezo wa kiungu wa kufanya mambo yaliyoshindikana kwa akili za kibinadamu. Yapo mambo ya kibinadamu ambayo akili za kibinadamu zimeshindwa kuyatatua hapo ndipo Upako wa Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kuyatatua.

Rejea, Biblia Takatifu, Kitabu cha Matendo ya Mitume 1:8, “Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Nabii Dkt.Mjuni ambaye ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliokirimiwa kipawa cha kipekee na kujazwa na Roho Mtakatifu, amekuwa akiachilia upako huo kwa maelfu ya watu ambao wamefungwa katika vifungo mbalimbali vya kishetani na baadaye huwa wanamshukuru Mungu kwa kutendewa matendo makuu ndani na nje ya Iringa Vijijini.

Amesema, siri ya mafanikio hayo inatokana na maombi ambayo amekuwa akifanyiwa na mkewe, Anitha huku na yeye akisimama imara katika kulisoma neno la Mungu, kufunga na kuomba kila siku ili Mungu azidi kumpatia nguvu zaidi ya kuwafungua walio vifungoni.

"Ukiwa na nguvu za Mungu chochote ulichonacho kinaweza kufanya maajabu, siku moja Nabii Tb Joshua (marehemu kwa sasa) wa Nigeria aliniambia mke wako awe anakuombea sana,mke wangu Anitha ni mchango kwenye upako huu, Mungu anamtumia kuniombea sana, hivyo ni funzo wake zetu manabii tusiwaache nyuma, kwani watu wote watakapokuwa wana vita na wewe ni mke wako pekee atakayebaki upande wako.

"Kila mtu ana neema yake,mwingine amepewa neema ya fedha ila sio mwaminifu,wewe hujapewa neema ya fedha ila ni mwaminifu,mwingine amepewa neema ya kufugua watu ila hana familia bora wewe hufungui watu ila una neema ya familia bora.

"Mwingine ana neema ya nguvu ila hana staha,wewe una staha ila huna nguvu,mwingine ana neema ya pesa ila amezuiliwa kula anachotaka,wewe huna neema ya pesa ila waweza kula chochote, Paulo alipewa mwiba asijivune zaidi kila mtu ana mwiba wake,kile unatamani kwa mwenzako huenda wewe unacho ambacho hana tofauti yeye ametambua neema yake wewe huitambui.

"Kuna watu unafikiri wana kitu kikubwa kuliko wewe ila wewe una kitu kikubwa, shida ni mtazamo tena hata kuliko wao siku hizi mtu anatukuzwa kuliko Muumba wake umaskini ni kitu kibaya tuukemee wapendwa,tuwekeze kwenye mambo mawili KUJIAMINI NA UAMINIFU,"amefafanua Nabii Dkt.Mjuni.

Wakati huo huo, Nabii Dkt.Mjuni amebainisha kuwa,"ukipigwa panapouma unaumia sana,na unapokuwa dhaifu shetani anashambulia,jitahidi kutokuwa dhaifu,kumbuka kuna kikomo kwa kila kitu,usipoteze matumaini kwa kile unapitia,kumbuka baada ya maradi mengi mvua inanyesha jitie moyo.

"Mungu hutuwazia mema, rejea Yeremia 29:11,hicho unachofanya ni hatua katika mwelekeo sahihi hata kama umeanzia katika hali ya udhaifu kiasi gani,itakusaidia ukijua hupaswi kupoteza ni agizo la Yesu, kwani watu hatari ni wale wasiokuwa na cha kupoteza,hautapoteza kazi, mtoto,mume,mke,biashara,na chochote unachokitegemea katika jina la Yesu pekee lipitalo majina yote makubwa tuyajuayo,"amefafanua Nabii Dkt.Mjuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news