Mama Ongea na Mwanao yawapa tabasamu yatima

NA DIRAMAKINI

MAKUNDI mbalimbali ya watoto wenye mahitaji maalum katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam yamefikiwa na misaada kutoka Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 19, 2023 na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Steven Mengele (Steve Nyerere) wakati akikabidhi sehemu ya misaada hiyo,lengo likiwa ni kuwashika mkono watoto hao wakiwemo yatima.

Amesema, katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, watu wengi wamekuwa wakiwashika mkono yatima kwa kuwafuturisha, lakini wao wameamua kuwashika mkono kupitia hijabu 500, michele, mafuta na misahafu.

“Tumekuja kuwashika mkono watoto yatima wa Wilaya ya Kinondoni, na msaada huu tunautoa kwa vituo vitatu, ambavyo ni Faraji, Chakuwama na Upendo Center,”amesema.

Pia, taasisi hiyo imemshika mkono Mama Mzazi wa msanii wa vichekesho nchini Zimwi kwa kumpatia zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, imemkabidhi michele, mafuta na kumhakikishia kwamba wapo pamoja naye kuhakikisha mwanaye anarudi katika hali nzuri kiafya na kurejea katika shughuli zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news