Michezo ya Kombe la Mei Mosi 2023 yazinduliwa rasmi Morogoro

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Mwasa amesema michezo ni muhimu katika kuimarisha afya za wafanyakazi mahala pa kazi ili waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi na kuongeza tija kazini.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo Aprili 20, 2023 wakati akizundua rasmi Michezo ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea katika viwanja mbalimbali Manispaa ya Morogoro kwa kuwahusisha wafanyakazi wa umma na sekta binafsi.

“Mfanyakazi asiye na afya bora na legelege kwakweli hataweza kutoa huduma bora na kuzalisha kwa tija kwa kuwa mwili wake umekosa mazoezi, michezo mahala pa kazi husaidia kujenga afya na mahusiano mema miongoni mwa wafanyakazi,” amesema Mkuu wa Mkoa.

Akinukuu Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa ya mwaka 1995, Mkuu wa Mkoa Mhe. Mwasa amesema sera hiyo inasisistiza katika taifa linaloshiriki michezo ili kujenga uhusiano, uelewanona mshikamano wa kitaifa kupitia michezo mbalimbali na kuhimiza kuwa michezo siyo suala la hiyari, bali ni takwa la kisheria katika kukuza uchumi na kuboresha afya za wananchi.

Ameahimiza vyama vya wafanyakazi na waajiri kulipa kipaumbele suala la kufanya michezo mahala pa kazi na kuweka msukumo na kuruhusu michezo mahala pa kazi.

Aidha, amewakumbusha viongozi kutenga bajeti kwa ajili ya michezo na kutenga muda kwa wafanyakazi wao kufanya michezo ili wafanyakazi wawe na utimamu na umadhubuti wa mwili na kuongeza tija kazini.

Amesema kuwa, kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Miaka Miwili ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Imeimarisha Michezo na Kuongeza Ufanisi Kazini, Kazi Iendelee” na kusema kuwa ni ukweli usiopingika mwanamichezo kasi yake ya kufanyakazi ni nzuri na kusisitiza kuwa wafanyakazi wameelewa dhana ya michezo na kugundua kuwa michezo inaimarisha afya na kuuweka mwili imara na matokeo yake kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wafanyakazi.

Aidha, wanahabari nao ni wanamichezo wapaswa kushiriki michezo hiyo ya Mei Mosi mwakani kupitia chama chao, Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (JET), Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kuwa wafanyakazi ni watu wote kwa kuwa hata mtu mwenye wazo la kufanya kazi ya kuajiriwa hata kujiajiri ni mfanyakazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amesema kuwa mashindano hayo yanaundwa mashirikisho manne ambayo ni SHIMIWI linashirikisha Wizara na Idara za Serikali, SHIMUTA linahusisha mashirika ya Umma, taasisi na makampuni binafsi, SHIMISEMITA linahusisha Serikali za Mitaa na BAMATA linahusisha majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Dkt. Mkanachi amesema michezo hiyo inashirikisha timu kutoka mashirikisho yote manne ambayo yalianzishwa na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mwaka 1967 na mashindano hayo yanaendelea mpaka sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news