Mvua yaua watoto 37 nchini

NA ABEL PAUL-Tanpol

JESHI la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi wanaotumia vibaya mitaandao ya kijamii hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendela kunyesha ambapo limesema kuanzia Januari hadi Aprili, mwaka huu kumejitokeza matukio ya watoto kufa maji kwa kusombwa na maji maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo watoto 37 wameripotiwa kupoteza maisha.
Akitoa taarifa hiyo leo Aprili 29,2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamisha Msadizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema kuwa, baadhi ya mikoa ambayo matukio hayo yameripotiwa ni Arusha, Dar es Salaam, Katavi, Kilimanjaro, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Pwani na Rukwa.

SACP Misime amebainisha kuwa, matukio hayo kuna baadhi ya wazazi wanashindwa kuwalinda watoto wao ambapo amesema, jeshi hilo litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kushindwa kutekeleza wajibu wa kisheria na kusababisha mtoto kupata madhara.

Pia amesema kuwa, Jeshi la Polisi nchini linatoa tahadhari na onyo kwa wale wachache wanaoendelea kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kusababisha hofu,taharuki kwa wananchi.
Amesema kuwa, kuna taarifa imerushwa hivi karibuni ikionesha gari aina ya Land Cruiser hard top ikisombwa na maji ambapo mhalifu aliyetengeneza uongo huo aliandika tukio hilo limetokea muda mfupi huko Arusha ambapo amebainisha kuwa tukio hilo lilitokea mwaka jana nchini Sudan Kusini.

SACP Misime amesema, jamii iendelee kuwakumbusha watumiaji vibaya wa mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya binadamu wenzao wana magonjwa na wanapopata taarifa za kushtua kama hizo wanaweza kupata madhara makubwa zaidi hata kupoteza maisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news