Rais Dkt.Mwinyi aendelea kusisitiza dhamira njema ya Serikali kwa ustawi bora wa wananchi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Julai 10,2021 alifanya ziara kwa wakazi wa nyumba chakavu za Kilimani ili kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano wake na waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao umefanyika leo Aprili 29, 2023 Ikulu jijini Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali itasubiri mapendekezo kutoka kwa kamati ya wakaazi wa Kilimani ambayo itasimamia maoni ya wananchi na baadae yawasilishwe serikalini. 

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amefananua kuwa lengo la Serikali ni kuendelea kutoa huduma bila malipo na kuboresha huduma za afya kwa sekta binafsi ili kuleta ufanisi na uharaka wa huduma hizi za Afya ikiwemo huduma ya vipimo vya maabara, mionzi, utoaji wa huduma za chakula, usafi na kutoa dawa.

Pia, Dkt. Mwinyi amezungumzia mkataba wa uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar kwa kampuni ya RAK GAS, ambayo iliingia mkataba na Serikali ya awamu iliyopita. 

Kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba ya awali ikiwemo kuchimba kisima cha kwanza kwa mujibu wa mkataba na hatua nyinginezo.

Hivyo, Serikali imewataka RAK GAS kuandika barua kueleza hatua waliyofikia kuhusu kuendelea na mkataba huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news