Rais Dkt.Mwinyi kuteta na waandishi wa habari kesho


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi atakutana na waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kesho Aprili 29, 2023, saa: 4 asubuhi, Ikulu jijini Zanzibar.

Hotuba yake italenga kutoa maelezo na kujibu maswali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake.

Mikutano ya aina hii ya kila mwisho wa mwezi ina lenga kuboresha uhusiano kati ya Serikali, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news