Rais Dkt.Samia aridhia ajira 21,200 kada ya afya na elimu

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ametoa nafasi za ajira 21,200 katika kada ya elimu na afya.

Katika kada ya elimu ni watumishi 13,130 watakaofundisha katika shule za msingi na sekondari na katika kada ya afya ni watumishi 8070 watakaofanyakazi katika hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati nchini.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 12, 2023 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa OR-TAMISEMI, Mheshimiwa Angella Kairuki.

Mheshimiwa Waziri Kairuki amesema mwisho wa maombi hayo ni tarehe 25 Aprili,2023 saa 05:59 usiku.

“Kwa kada ya elimu waombaji wawe ni wale waliohitimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2022 na afya wawe wasiozidi miaka 45 na wanatakiwa kutuma maombi kuanzia leo tarehe 12,04,2023 na mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25, 4, 2023 saa 05:59 usiku,”amefafanua Mheshimiwa Waziri Kairuki.

Pia, kwa upande wa watumishi wanaoendelea kujitolea,Mheshimiwa Waziri Kairuki amesema, OR-TAMISEMI ina orodha yao ambapo amesisitiza waombe ajira kupitia tangazo hilo ili wapate nafasi ya kuingia katika mfumo wa ajira za Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news