Rais Dkt.Samia avunja Bodi ya TRC,atengua uteuzi TGFA na kutoa maagizo kwa makatibu wakuu, watendaji wote kuhusu Ripoti ya CAG

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Aidha, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 9,2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news