Rais wa Kenya aitaka Afrika kuimarisha juhudi za pamoja kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

NAIROBI- Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt.William Ruto ameiomba Afrika kufanya juhudi za pamoja ili kushinda vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Amesema bara limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na athari zake mbaya. Amebainisha kuwa, uundaji upya wa kitaasisi na urekebishaji wa uchumi unaotokana na mabadiliko hayo utaiweka Afrika kama nguvu kuu ya uchumi wa kijani kibichi duniani.

"Ingawa mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio la kuwepo kwa ulimwengu wote, kuna sababu nzuri kwa taasisi na uongozi wa Afrika kuendesha ajenda ya kupunguza athari zake," alisema.

Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto alikuwa akizungumza wakati wa Kongamano la 3 la Kikanda linalofahamika kama Regional Symposium on Greening Judiciaries in Africa katika Hoteli ya Safari Park Kaunti ya Nairobi.

Rais alisema maafa ya hali ya hewa yanayokuja ni ya kutisha sana kwa Afrika, ambayo inaingia kwenye njia mpya ya kuimarisha amani na ustawi wa kiuchumi.

Pia, Mheshimiwa Rais aliuambia mkutano huo kuwa licha ya ukweli kwamba Afrika imejikita katika kukabiliana na umaskini na ukosefu wa usawa, njia ya uchafuzi wa mazingira sio chaguo jema.

Aliipongeza Idara ya Mahakama kwa kuchukua nafasi ya mbele katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. "Mahakama zetu zitaamua kama taasisi za Afrika zipo na ziko tayari kushughulikia majukumu makubwa ambayo mustakabali wa kijani unajumuisha."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news