Ujenzi Uwanja wa Ndege Msalato washika kasi

NA MWANDISHI WETU

UTEKELEZAJI wa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato jijini Dodoma unaendelea kwa kasi ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 18.5 huku ukitarajiwa kukamilika mwezi Aprili, mwaka 2025.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mhandisi wa Mradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani humo, Mhandisi Colman Gaston wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema utekelezaji wa mradi huo utahusisha sehemu mbili za ujenzi.

Mhandisi Colman amesema sehemu ya kwanza ya ujenzi unahusisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo sehemu ya kurukia ndege (run way), sehemu za kupaki ndege.

“Mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato unahusisha ujenzi wa sehemu ya kurukia ndege (run way), sehemu za kupaki ndege (tax way) na maegesho (apron), Pia mradi huo utahusisha ujenzi wa fensi na miundombinu ya umeme pamoja na miundombinu ya kuzima moto,"alisema Mhandisi Colman.

Kuhusu sehemu ya pili ya utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Colman amesema utahusisha ujenzi wa jengo la abiria (terminal building), mnara wa kuongozea ndege (observation tower) ambapo katika sehemu hii utekelezaji wake unafanywa na mkandarasi China Beijing na utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 194”.

Kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato jijiji Dodoma kunatajwa kuwa chachu ya kubadili mandhari ya jiji hilo, kwani ndege zote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Ulaya zitatua moja kwa moja katika uwanja huo badala ya Dar es Salaam kama ilivyozoeleka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news