Yanga SC yazidi kuwa tishio Afrika, yaichapa Rivers United mabao 2-0

NA DIRAMAKINI

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa kupitia Kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga SC imeichapa Rivers United 2-0 kupitia mabao yaliyofungwa na Fiston Mayele katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Ni katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao umepigwa leo katika Uwanja wa Venue Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria.

Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 73, ingawa ilibidi refa Abongile Tom wa Afrika Kusini akajiridhishe kwenye VAR na la pili dakika ya 81 mara zote akimalizia pasi ya beki na nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto.

Aidha, kipindi cha kwanza Yanga SC iliingia ikicheza mfumo wa mabeki watano ambapo upande wa beki wa kushoto alicheza Joyce Lomalisa Mutambala ambaye alikuwa anapanda na kushuka vilevile kwa upande wake Djuma Shabaan.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko kuanzia kwenye mfumo kutoka 3-5-2 na kuwa 4-4-2 na kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ambapo mabadiliko hayo yalizaa matunda, kwani yalisaidia kupata matokeo hayo.

Hata hivyo, timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news