Balozi wa Norway anayemaliza muda wake nchini amuaga Rais Dkt.Mwinyi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo ametembelewa na Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen aliyefika Ikulu kumuaga baada ya kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano akiiwakilisha nchi yake hapa Tanzania.
Katika mazungumzo yao, Rais Dkt.Mwinyi ameshukuru uhusiano uliopo kati ya Norway na Zanzibar katika sekta ya afya na nishati ya umeme.
Balozi Elisabeth baada ya kuhudumu Tanzania kwa muda wa miaka hiyo anarejea Norway akiwa mstaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news