DJ Maphorisa mbaroni kwa kumshambulia mpenzi wake

NA DIRAMAKINI

MTAYARISHAJI wa Amapiano na mpiga nyimbo katika klabu, DJ Themba Sonnyboy Sekowe anayejulikana zaidi kama DJ Maphorisa amekamatwa Jumapili ya Mei 7, 2023 mchana kwa madai ya kumpiga mpenzi wake Thuli Phongolo.

Tukio la kushambuliwa lilifichuliwa katika taarifa iliyotolewa na Phongolo katika Kituo cha Polisi cha Sandton nchini Afrika Kusini.

Unyanyasaji huo wa kijinsia unadaiwa kutokea katika nyumba ya mwigizaji wa zamani wa Generations: The Legacy huko Sandton, Johannesburg.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo City Press imeona, tukio hilo lilianza wakati Phongolo alipomkabili Maphorisa kuhusu ugomvi wao wa usiku uliopita kwenye tamasha alilopangiwa kutumbuiza.

Haijabainika iwapo wawili hao walipangiwa kutumbuiza pamoja katika ukumbi mmoja, lakini kulingana na taarifa ya Phongolo, walianza kuzozana mbele ya watu.

“Siku ya Jumapili, Mei 7, 2023 nilikuwa nyumbani kwangu na mpenzi wangu, Themba Sonnyboy Sekowe, anayejulikana zaidi kama DJ Maphorisa. Nilimuomba ili tuzungumzie mabishano yetu yaliyotokea usiku wa kuamkia jana wakati wa tafrija yake,” alisema Phongolo katika taarifa hiyo.

Aliwaambia polisi kwamba alipokuwa akizungumza Maphorisa, alizidi kuwa mkali na kumpiga kofi usoni. Alielezea jinsi alivyomgeuza kuwa ngoma kwa kuanza kumpiga ngumi baada ya kofi hilo usoni.

Phongolo kwa undani alisema: "Alizidi kuwa mkali na kuanza kunipiga ngumi kifuani." Aliwaambia zaidi polisi kwamba alimpeleka kwenye baraza baada ya kumpiga wakiwa ndani ya ghorofa.

"Alinishika na kunipeleka kwenye baraza, na kunishika shingoni kwa hasira." Phongolo aliongeza kuwa aliendelea kumpiga kwa kiwiko kwenye baraza wakati wakigombania simu yake ambayo alimnyang’anya.

Mwigizaji huyo na DJ alisema, baada ya kumpa simu hiyo, alimpigia meneja wake ambaye alimpeleka kituo cha polisi kumfungulia kesi ya unyanyasaji wa nyumbani.

Kwa mujibu wa polisi waliomuona katika kituo cha polisi, Phongolo alipata michubuko mikubwa shingoni.Katika maelezo yake, alisema alipata michubuko kwenye shingo, kifua, mikono na shavu la kulia.

Haijabainika ni nini kilizua mabishano hayo, lakini vyanzo vinasema wawili hao wamekuwa na matatizo makubwa katika uhusiano wao.Chanzo cha habari katika tasnia ya muziki kilidai kuwa, hiyo haikuwa mara ya kwanza wao kugombana vikali.

"Walipigana mapema Desemba baada ya tuhuma za kutokuwa na uaminifu. Walipigana tena mwezi uliopita, lakini hawakufika kituo cha polisi,” kilifichua chanzo hicho.

Maphorisa anatarajiwa kufika katika Mahakama ya Randburg leo Jumatatu kujibu mashtaka ya shambulio. Chanzo cha karibu cha wawili hao kilisema Maphorisa aliomba kuwaita mawakili wake alipokuwa ndani ya sero za polisi alikozuiliwa.“Alikuwa akijaribu kujadiliana ili kupata dhamana ya polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news