Dkt.Yonazi aongoza kikao cha makatibu wakuu cha nishati safi ya kupikia

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi Ngazi ya Makatibu Wakuu kilicholenga kupitia utekelezaji wa maboresho ya rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 yaliyotolewa na Waziri Mkuu wiki moja iliyopita Machi 23, 2023 mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jim Yonazi akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma.

Dkt.Yonazi ameongoza Kikao hicho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Naibu Katibu Mkuu Nishati Bw. Athuman Mbuttaka akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia kilichofanyika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehusisha Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na Wajumbe wa Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia kilichofanyika Machi 30, 2023 jijini Dodoma.
Dkt.Yonazi amesema kuwa, kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa maboresho na maelekezo yaliotolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, alipokutana na Mawaziri na Naibu Mawaziri Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho Jijini Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Mara baada ya Makatibu Wakuu hao kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi safi ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 na Rasimu ya Mpango Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, itawasilisha kwa Waziri Mkuu tarehe 31 Machi 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news