Dkt.Yonazi ataka elimu itolewe kupinga unyanyapaa kwa WAVIU

NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kuwa elimu inapaswa kuendelea kutolewa katika jamii kupinga vitendo vya unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI nchini ili kuendelea kuunga mkono mapambano dhidi ya UKIMWI katika Taifa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Utaribu) Dkt. Jim Yonazi akipokea nyaraka kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bw.Deogratius Rutatwa mara baada ya mazungumzo yao ya kikazi leo Mei 9, 2023 jijini Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt.Jim Yonazi mapema leo Mei 9, 2023 alipokutana na uongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI nchini (NACOPHA).
Akieleza jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, Dkt. Yonazi amesema ipo mikakakti madhubuti ya kuendelea kuelimisha umma kuhusu kupinga masuala ya unyanyapaa kwa WAVIU huku akiiasa jamii kuwa mstari wa mbele katika jitihada hizo.

“Afua mbalimbali za masuala ya UKIMWI zimeendelea kuonesha jitihada za Serikali katika mapambano haya, nitoe rai elimu iendelee kupewa kipaumbele ili kupinga unyanyapaa kwa WAVIU,”amesema Dkt.Yonazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Utaribu) Dkt. Jim Yonazi akioneshwa nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bw.Deogratius Rutatwa walipomtembelea na kufanya mazungumzo katika Ofisi yake Jijini Dodoma.

Dkt.Yonazi ameongezea kuwa, ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa NACOPHA ili kuhakikisha sifuri tatu zinafikiwa ifikapo 2030.
Mratibu wa Dawati la masuala ya UKIMWI Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Adela Mpina akizungumza jambo wakati wa kikao cha ujumbe kutoka NACOPHA.

“Tutaendelea kushirikisha wadau mbalimbali lengo kuhakikisha tunayafikia malengo, na ofisi yangu ipo tayari kutoa ushirikiano wakati wote kuhakikisha masuala yote ya uratibu yanatekelezwa vizuri ili kuendelea kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuhakikisha tunaondoa unyanyapaa katika jamii,”amesisitiza.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bw.Deogratius Rutatwa akieleza majukumu ya ofisi yake kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Utaribu) Dkt. Jim Yonazi walipomtembelea ofisini kwake Mei 9, 2023 Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Bw.Deogratius Rutatwa amepongeza jitihada za Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika kurahisisha utendaji wa Baraza hilo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Utaribu) Dkt. Jim Yonazi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA), mara baada ya mazungumzo yao Mei 9, 2023 Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

“Hadi sasa tuna jumla ya wanachama laki sita na elfu sabini na mbili pamoja na vikundi vya WAVIU 3769 katika shughuli za kujipatia maendeleo yao ambavyo vinatoa fursa kushiriki katika shughuli mbalimbali na tunatumia kuhamasisha watu kuendelea kupima virusi vya UKIMWI na utumiaji wa dawa kwa wanaogundulika na maambukizi,”amesema Deogratius.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news