Ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi yakutana na Katibu Mkuu Dkt.Yonazi

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amekutana na ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya AFDP pamoja na Wataalam na kufanya nao mazungumzo ofisini kwakejJijini Dodoma leo Mei 9, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (mwenye suti ya blue) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP walipomtembelea na kufanya mazungumzo katika Ofisi yake jijini Dodoma leo Mei 9, 2023.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Katika mazungumzo yao, Katibu Mkuu, Dkt.Yonazi alieleza kuwa Serikali tayari inatoa ushirikiano wa hali ya juu katika kutekeleza program hiyo na pia, kwa wakati inaainisha masuala mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika utekelezaji wake na kutafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu za Serikali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP walipomtembelea na kufanya mazungumzo katika Ofisi yake jijini Dodoma leo Mei 9, 2023.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa program hiyo nchini Bw. Robson Mutendi alisema,ujumbe huu maalum wa ukaguzi wa maeneo ya mradi, utatembelea katika baadhi ya maeneo ambayo mradi unatekelezeka ikiwa ni njia mojawapo ya kuona na kuainisha maeneo yenye mapungufu, ili kufanyiwa kazi na kufikia malengo, na kuomba ushirikiano katika utendaji ili uweze kuleta matokeo tarajiwa.
Mwakilishi Mkazi wa programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya AFDP nchini Bw. Robson Mutendi akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi walipokutana naye Mei 9, 2023 jijini Dodoma.

Baada ya mazungumzo hayo mahususi na Katibu Mkuu, Ujumbe huo pamoja na wataalam utakutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi na pia utambelea baadhi ya maeneo inapotekelezwa program hiyo ikiwa ni pamoja na mikoa ya Tabora, Geita , Lindi na Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news