Fei Toto awaangukia Watanzania

NA DIRAMAKINI

MCHEZAJI Feisal Salum maarufu kama Fei Toto baada ya juhudi zake kugonga mwamba mara mbili katika Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Klabu ya Yanga ametangaza kuomba msaada wa fedha kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Kimichezo (CAS).
Fei Toto ameyabainisha hayo kupitia taarifa aliyoichapisha katika kurasa zake za kijamii huku akiambatanisha na mfumo wa kumchangia aweze kufikia lengo la kupata zaidi ya dola 30.

"Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heros.

"Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS.
.
"Nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, Heshima na Haki zao. 

"Naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya kulipia gharama za kufungua Jjalada la kesi yangu CAS ili kupata haki yangu ya kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba.
.
"Tafadhali naomba unichangie ili nipate haki yangu itakayoniwezesha kutumikia kipaji changu na timu za Taifa (Tanzania na Zanzibar) katika namna tofauti kwa manufaa yangu na Taifa. Shangazi Fatma Karume na wanasheria wengine watafanya kazi bure.
"Unaweza kulipia kwa lipa namba (5406394 FEISAL SALUM) hapo pichani au kwa namba hii ya simu kwa kwa Tigo Pesa 067 912 8899 FEISAL SALUM ABDALLAH.NAOMBA UNICHANGIE,"amefafanua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news