Simba SC waendelea kujinoa

NA DIRAMAKINI

BAADA ya mapumziko wachezaji wa Simba SC wamerejea mazoezini kujiandaa na mechi mbili zilizozalia za Ligi Kuu ya NBC Tanzania BARA.

Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Mo Simba Arena jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ pamoja na wasaidizi wake.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wameonekana wapo kwenye hali nzuri.Michezo inayofuata utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania na Simba SC ambao utakaopigiwa Juni 6,2023 wakati wa mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Coastal Union Juni 9, 2023 na zote watakuwa nyumbani.

Post a Comment

0 Comments